Friday, 2 March 2012

Buriani kaka Seph Yusuph seph

Tarehe 9/02/2012  familai yetu tumeondokewa na
jembe letu muhimu sana kaka SEPH MDOE.

ki ukweli ni siku ngumu sana kwa kila mmoja wetu
 Kila utakazungumza naye ana kumbukumbu zake binafsi juu ya kifo cha kaka yangu huyu

kaka seph ni mtu mvumilivu sana
 muelewa
moja kati ya vijana ambao hawana makuu mbele ya vijana wenzake
 kaka mfano wako kuupata ni vigumu sana

















watu waliofika kwa ajili ya msiba wa kaka  yangu







 watu waliofika kujakumuaga kaka seph
wakiangalia gali lililobeba mwili wa kaka
likiondoka.






hili ndilo gari lililobeba mwili wa kaka seph mdoe












kwa heri kaka yangu mungu ailaze roho yako mahala pema peponi .
amin
ila kama una uwezo wa kutusikia

TULIKUPENDA  SANA

TUNAKUPENDA SANA

       NA
TUTAKUPENDA DAMA

KAKA MPENDWA.

Saturday, 18 February 2012

EMMANUEL MYAMBA AZINDUA RASMI CHUO CHAKE CHA FILAMU(TANZANIA FILM TRAINING CENTER,,TFTC)



Meza kuu,kutoka kushoto ni Baucha,Myamba,mwakilishi wa katibu mkuu Basata,na Makubi ambaye ni mratibu wa chuo hicho.
Ukisomwa ujumbe maalum wa mgeni rasmi toka Basata.
Kanumba  kama mmoja wa walezi na mshauri wa chuo hicho alipewa nafasi ya kusema machache kwa wanafunzi na tasnia kwa ujumla.
Wanafunzi wakiwa na uniform zao safi kabisa lakini pia humu ndio darasa lao,wanasoma katika air condition,
Bosi wa chuo Pastor Myamba akikabithiwa kibali toka Basata kama ishara ya kwamba anatambulika rasmi na mamlaka husika serikalini.
Wosia toka Basata...msipende kukatishana tamaa na kuharibiana,Basata ipo kwa ajili yenu na ndio walezi na washauri wakuu wenu.
Cheti cha usajili..
hongera sana  pastor myamba kwani huu ndio mwanzo wa maendeleo kwa tasnia yetu. 
 ushauri wangu kwako   jambo uliloanza si jepesi hata kidogo  usikatishwe tamaa na mtu yeyote kaza buti songa mbele baba. 

Friday, 17 February 2012

NINAPOAMUA KUTANGAZA MAHABA YANGU YA DHATI KWA "MENDE"...SEBASTIAN MAGANGA


TAMKO HILI LINAWEZA KUNIHUSISHA KWA KARIBU NA "UGONJWA WA AKILI"  KWANI KATIKA HALI YA KAWAIDA, NI JAMBO LA KUSTAAJABISHA PINDI AMBAPO, BINADAMU ANATAMKA BILA UOGA KWAMBA ANAMPENDA MENDE, UKITILIA MANAANI KWAMBA, KIDESTURI WADUDU HAWA WANAHUSISHWA NA UCHAFU.
 LAKINI KAMA WASEMAVYO WASWAHILI, A.KA. WAHENGA "HAKUNA UJINGA ULIOUJINGA MTUPU' TENA KAMA TUNGELIJUA KUTHUBUTU KUIGA MAISHA YA MENDE NI KUTHUBUTU KUCHUKUA MAARIFA AMBAYO YANAWEZA KUTUSAIDIA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,
KWA MFANO:

A] MENDE ANAUWEZO WA KUISHI KATIKA MAZINGIRA YEYOTE, IWE BARIDI KAAAALIIII AU JOTO LILILOKITHIRI, YEYE HUJIWEKA TAYARI KUTOKANA NA MAZINGIRA, KWANINI NA SISI TUSIJIANDAE KWA MIKIKI YA KIMAISHA? IL HALI MAISHA YETU YANAWEZA KUBADILIKA WAKATI WOWOTE? .

B] MENDE ANAWEZA KUISHI BILA KULA KWA MWEZI MZIMA, ANAWEZA PIA KUISHI BILA KUNYWA MAJI KWA WIKI NZIMA, KAMA VILE HAITOSHI HATA UKIMKATA KICHWA ANADUNDA HAI KWA SIKU 7....HAYO KWA BINADAMU HAYAWEZEKANI LAKINI KWA MIFANO HIYO CHA KUANGALIA HAPO NI KIWANGO CHA UVUMILIVU NA USHUPAVU WA MENDE, KWA KUIGA USHUPAVU NA UVUMILIVU  WAKATI TUNATAFUTA NJIA YA KUTIMIZA NDOTO ZETU, KUTATUSAIDIA SAANA KWANI  TUTALAZIMIKA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU NA KUBADILISHA MFUMO WETU WA KIMAISHA, NA JAPOKUWA ILE HALI ITUTUPA MATESO LAKINI, FARAJA YA MIPANGO YETU NA UVUMILIVU WETU, ITAZAA MATUNDA, WAINGEREZA WANASEMA WAZI WAZI NAMI SIBISHI "HARD WORK PAYS".

C] MACHO YA MENDE YANA LENSI KAMA 4000 HIVI, HIVYO KUMFANYA AWEZE KUONA PANDE ZOOOTE WAKATI MMOJA, ANTENNA ZAKE (ZIKO KAMA ZILE ANTENNA ZA TV ZILIZOPEWA JINA LA CHADEMA) INAWEZA KUWASAKA MENDE WENZAKE KWA URAHISI HATA KAMA WAMEJIFICHA FUTI SITA CHINI YA ARDHI, KWA MFUMO HUO TUNAWEZA KUJIFUNZA NAMNA YA KUTUMIA TEKNOLOJIA TULIOKUWA NAYO KWA MINAJILI YA KUTUPA TIJA ZAIDI KATIKA MAISHA YETU BINAFSI NA KIKAZI.
MWISHO KABISA NI KWAMBA MENDE ANA PAIR MBILI ZA MENO, YALE YA MDOMONI NA TUMBONI...SOMO KWETU HAPO NI LA MUHIMU SAANA , LAZIMA TUWE NA MPANGO WA AWALI NA MPANGO SAIDIZI IWAPO MPANGO WA AWALI UTAFELI TUTACHAGUA KUTMIA MPANGO SAIDIZI...KWA MIFANO HII NADHANI UTAJUINGA NAMI KATIKA KUELEKEZA MAHABA YA DHATI KWA MDUDU "MENDE"
(NYONGEZA NI KWAMBA MENDE NI KITOWEO SAAAFI KATIKA NCHI NYINGINE)

KANYE WEST ASEPA NA TUZO YA GRAMMY "BEST RAP ALBUM"


Kanye West ameondoka na ushindi mkubwa katika upande wa hiphop, jana katika tuzo za 54 za Grammy. kanye alienda home na tuzo ya Rap Album Of The Year kwa My Beautiful Dark Twisted Fantasy album.
Kanye pia ameondoka tuzo ya Best Rap Collaboration kwa “All Of The Lights” akiwa na Rihanna, Fergie, Elly Jackson and Elton John.
collaboration yake pia  “Otis” na Jay-Z and Otis Redding pia imechukua Best Rap Performance.
Jay Z na kanye kwa pamoja licha ya kutoa bonge moja la album "Watch the throne" wameskip the Grammy awards.
washindi wengine ni pamoja na Chris Brown, ambae ameshinda tuzo ya best R&B album kwa F*A*M*E na Cee Lo Green, ambae alishinda Traditional R&B Vocal Performance na Best R&B Song kwa “Fool For You” na Hallim & Jack Splash.
Adele pia ameondoka nyumbani na tuzo 7 za grammy kwa album yake inayoitwa album 21 na hit single “Rolling In The Deep,”

this is my pretty girl (sabrina )

Ki ukweli ninayo furaha kubwa sana   kwa mwanagu kutimiza 
siku arobainai  .
 ni siku ambayo niliingoja sana katika maisha yangu 
japo nimepata bahati mbaya ya kuondokewa na kaka yangu kipenzi 
SEPH MDOE . bado moyo wangu unafarijika kwa hili 
 R.I.P  my brother najua ya kuwa wewe ni moja kati ya waja bora
 mbele ya  mungu kwani ulijitahidi kufanya ibada kwa karibia 
 maisha yako yote, mungu atakulaza mahala pema peponi 
 
 you know 
 
I LOVE U SO MUCH 

  ila usijali kaka mimi naamini ntakuwakilisha katika kila jambo ulilo jaribu kulifanya mimi nitakuwepo kulimalizia 
 
 INSHAALLAH 

 umeondoka lakini  amekuja 


SABRINA 
 
 unamjua SABRINA 

 kama una nafasi ya kumuombea aje awe moja ya watu wakubwa kwenye 
 dini yetu INSHAALLAH 
nampenda sana 

SABRINA 




 

Monday, 24 January 2011

naomba nizungumze kitu.

Ndugu zangu nakuja kwenu leo kuzungumza nanyi  ili kila mmoja wenu anielewe, najua kila mmoja anajua vile ambavyo sifurahii maisha haya ambayo ninayo.
tatizo nililonalo mwenzenu sijui namna ambayo naweza kutoka katika tatizo hili
 nimejaribu kufikiria  kadri niwezavyo lakini akili yangu inagoma.

 kati ya  jamaa zangu  ama ndugu zangu  wengi  wamepiga hatua kutoka   moja kwenda nyingine kwa msaada wa mawazo yangu .
 jamani ndugu , jamaa na marafiki naomba mnisaidie ili niweze kutoka katika dimbwi hili la matope ambalo kimsingi naona nimeshafika  shinngoni bado kidogo sana kabla ya kuzama na kupotea kabisa.
hofu yangu ni kwamba kichwa changu ni kati ya vichwa vichache sana lakini kinaweza kisitumike kabisa kutokana na  ukosefu wa imani juu yangu .
 sijui ni kwa nini watu hawana imani na mimi?
 hata hivyo si wote ni braza wangu mkubwa  ambae haniamini kwa chochote .
 kwa kweli depretion  zote   ndani ya moyo wangu zinakuja  kwa ajili yake  kwani nimekua  na tatizo kubwa akilini  mwangu    ambalo ni kutafuta  kukubalika mbele yake  kitu ambacho sidhani kama kitakuja kutokea,
 ni sawa na kukimbiza kimvuli chako ukifikiria kwamba ipo siku utakikamata.
inaniuma sana.  

Sunday, 23 January 2011

milton keynes central

enzi zile nikiwa kwenye jiji la watu mk ambako inapatikana
  mk dons