
nimejaribu kufikiria kadri niwezavyo lakini akili yangu inagoma.
kati ya jamaa zangu ama ndugu zangu wengi wamepiga hatua kutoka moja kwenda nyingine kwa msaada wa mawazo yangu .
jamani ndugu , jamaa na marafiki naomba mnisaidie ili niweze kutoka katika dimbwi hili la matope ambalo kimsingi naona nimeshafika shinngoni bado kidogo sana kabla ya kuzama na kupotea kabisa.
hofu yangu ni kwamba kichwa changu ni kati ya vichwa vichache sana lakini kinaweza kisitumike kabisa kutokana na ukosefu wa imani juu yangu .
sijui ni kwa nini watu hawana imani na mimi?
hata hivyo si wote ni braza wangu mkubwa ambae haniamini kwa chochote .
kwa kweli depretion zote ndani ya moyo wangu zinakuja kwa ajili yake kwani nimekua na tatizo kubwa akilini mwangu ambalo ni kutafuta kukubalika mbele yake kitu ambacho sidhani kama kitakuja kutokea,
ni sawa na kukimbiza kimvuli chako ukifikiria kwamba ipo siku utakikamata.
inaniuma sana.
No comments:
Post a Comment